Sunday, 5 June 2016

Matukio Siku Mwenge Ulipozuru Njinjo

Y
Malenga wakighani shairi la rushwa mbele ya mwenge wa uhuru. Kutoka kulia ni Mwanjaa Machungu, Bahati Mpakandunda na Aida Likwita
SLO Bi. Bofu akitoa maelekezo kwa walimu kabla kwaya ya shule haijaingia kutumbuiza.

Liyanga naye alikuwepo kwenye msafara akiburudisha japo aliwatia hasira mashabiki wa simba
Makamu mkuu wa Shule Mwl. Kapagi akipata picha ya pamoja na wanafunzi baada ya kupokea cheti cha klabu za Kupambana na rushwa ambapo kila mwanafunzi aliwakilisha shule moja kutokana na wahusika wa shule nyingine kutokuwepo, kutoka kulia ni Lawama Kitupa(Njinjo), Zulfa Ligunda (Miguruwe) na Fadhili Kichwilili (Mitole)
Mkuu wa Shule Mwl. Mmbaga(Kulia) na Mwl mwandamizi Michezo Mwl. Baraka Bunyinyiga wakipata picha ya pamoja baada ya kupokea vyeti.
Afisa utamaduni(W) Bw. Mtule akihojiana na mwanafunzi Saidi Kindumba baada ya kutamba vizuri kwenye ngonjera ya Malaria akivaa vema uhusika wa mzee viwanja vya shule ya msingi Njinjo mahali ulipalala mwenge.
Kwa mbali kwaya Ikitumbuiza mbele ya mwenge na pembeni Liyanga akinogesha zaidi kuongeza radha ya tukio


Ujio wa mwenge ulifanya viunga vya shule ya sekondari Njinjo kupambwa kwa chokaa hivyo kuwa na mwonekano wa kipekee.

Matukio haya yanahusu ujio wa mwenge shule ya sekondari Njinjo siku ya tarehe 25/05/2016 kuzindua klabu za kupambana na rushwa kwa shule za sekondari Ninjo, Mitole na Miguruwe.

Welcome note

Dear reader
Am happy to welcome you at our official blog for Njinjo Secondary School. The School which is found at Kipindimbi village, Njinjo ward, Kilwa district in Lindi Region. This site will be responsible for providing school information and areas around the school. The blog will be publishing information by either English or Swahili languages depending on the aim of information and targeted audience.

We are building new Njinjo, 
Mr. Kapagi P
School IT Director
IT Department