Shule ya sekondari Njinjo inao ushirikiano madhubuti na viongozi mbalimbali ili kuchochea maendeleo. Hapa tumetembelewa na Ndg. Selemani Mkangila-Katibu wa Mbunge wa Kilwa kask. akiwa ameambatana na Mratibu Elimu Kata Mwl Martin Mmbaga kukagua miundombinu ya shule hasa choo ambacho kimechakaa.
Mwl Mageni akionyesha matumizi ya kidumu mchirizi
Mkuu wa shule sekondari Njinjo akitoa maelezo juu ya mahitaji ya choo na idadi ya matundu yanayohitajika
Jengo la choo kinachohitaji kubadilishwa
Njinjo Secondary School is located at Kipindimbi village, Njinjo ward, Kilwa district in Lindi Region 96kms from Kilwa Masoko our District headquarters and 2kms from Nangurukuru-Liwale road.
Saturday, 26 August 2017
NJINJO DARASANI: MASOMO YA SAYANSI KWA NJIA YA MJADALA
Shule ya sekondari Njinjo tayari inao walimu wa masomo ya sayansi. Wanafunzi wengi wanachukulia masomo ya sayansi kuwa ni magumu, changamoto hii ni kubwa sana shule ya sekondari Njinjo kwa kuzingatia kuwa miaka ya nyuma hakukuwepo kabisa walimu wa masomo hayo.
Kukabili changamoto hiyo Walimu hubuni njia mbalimbali za kurahisisha shughuli ya ujifunzaji.
Leo nakuletea Mwl January Rwebugisa mwalimu wa masomo ya Kemia na Jiografia. Yeye wakati mwingine hujitenga na wanafunzi wake chini ya mti na kuwa na mjadala katika baadhi ya mada. Njia wanafunzi huifurahia sana na zaidi kutokana na uchache wa wanafunzi. Sifa kubwa ya Mwl Rwebugisa ni umahiri na kufanya mambo kwa ukamilifu na ubunifu wa juu sana. Tazama alivyo nadhifu na joho lake(Kumbuka yeye huwa mwalimu na mtaalamu wa maabara kwa wakati mmoja)

SHUGHULI YA USAFI WA MAZINGIRA YA SHULE KILA ASUBUHI
Suala la usafi shule ya sekondari Njinjo limepewa nafasi ya pekee. Taaluma lazima iende sambamba na mazingira safi ya kujifunzia. Hivyo basi ukifika Njinjo utajionea jinsi wanafunzi wake walivyo na bidii ya kuwahi kufika shule na kufanya usafi, walimu pia husimamia ipasavyo suala la usafi. Katika picha utajionea mtawanyiko wa wanafunzi wakifagia maeneo mbalimbali ya shule.
Karibu Njinjo, ujipatie mema.
Subscribe to:
Posts (Atom)