Saturday, 26 August 2017

NJINJO DARASANI: MASOMO YA SAYANSI KWA NJIA YA MJADALA

Shule ya sekondari Njinjo tayari inao walimu wa masomo ya sayansi. Wanafunzi wengi wanachukulia masomo ya sayansi kuwa ni magumu, changamoto hii ni kubwa sana shule ya sekondari Njinjo kwa kuzingatia kuwa miaka ya nyuma hakukuwepo kabisa walimu wa masomo hayo.

Kukabili changamoto hiyo Walimu hubuni njia mbalimbali za kurahisisha shughuli ya ujifunzaji.

Leo nakuletea Mwl January Rwebugisa mwalimu wa masomo ya Kemia na Jiografia. Yeye wakati mwingine hujitenga na wanafunzi wake chini ya mti na kuwa na mjadala katika baadhi ya mada. Njia wanafunzi huifurahia sana na zaidi kutokana na uchache wa wanafunzi. Sifa kubwa ya Mwl Rwebugisa ni umahiri na kufanya mambo kwa ukamilifu na ubunifu wa juu sana. Tazama alivyo nadhifu na joho lake(Kumbuka yeye huwa mwalimu na mtaalamu wa maabara kwa wakati mmoja)



No comments:

Post a Comment